tangazo hapa
Malengo ni nini.Malengo ni usafiri wa kutimiza ndoto zako.Mtu aweza kuwa na ndoto nyingi katika maisha na ili azitimize ni lazima aweke malengo yake,mfano mtu una ndoto ya kumiliki gari zuri,nyumba nzuri,mke mzuri, biashara etc ni lazima uweke malengo yako vizuri ili utimize ndoto zako kwa mfano ufanye kazi kwa bidii ili uongeze kipato chako.SABABU ZA KUTOTIMIZA MALENGO
1.Kutanguliza kushindwa.Baadhi ya watu kabla hawajafanya kitu wanawaza hawatofanikiwa mwishowe wanaacha kufanya kile kitu walichokusudia kukifanya mfano.mtu alitaka kufuga kuku kibiashara mwenyewe akajiwazisha je kuku wakifa,nikikosa masoko.
2.Kuomba ruhusa.Huu ni ugonjwa wa watu wengi hutokea pale mtu kabla hajafanya jambo ni lazima aombe ruhusa kwa mzazi,mwenza wake ,ndugu jamaa au rafiki .Watu wengine wana fikra mgando na siku zote wapo kwa ajili ya kukatiza watu tamaa ukiendelea kuwafatiza hutofanikiwa kamwe .Kama una mtaji wako,kama unakipaji chako cha sanaa mbalimbali kuimba, ufundi, mchoraji,muamasishaji wewe anza usitake kuomba ruhusa mwishowe unakatishwa tamaa .
3.Uvivu. Jamani watu wengi ni wavivu hususani katika kutekeleza mambo ya kimaendeleo tumebaki nitaanza mwakani kulima ikifika hulimi yani maneno mengi vitendo sifuri.
tangazo hapa
