tangazo hapa
Dawa ya michepuko kwa mwanamke au mwanaume
Michepuko ni kitendo cha kutoka nje ya ndoa mwanamke au mwanaume.Ndoa nyingi hukumbwa na tatizo hili na kupelekea ndoa kuvunjika.Tatizo ni kubwa na kupelekea watoto kuachwa katika mazingira magumu baada ya wazazi kutengana.Sababu za mume au mke kuchepuka.
ugumu wa maisha,uchafu,lugha mbaya kwa mwenza,utegemezi,ulevi,uchochezi wa ndugu,matendo machafu,makosa sugu,kuingia katika mahusiano kwa sababu ya Pesa,uzuri etc
Suluhisho la Michepuko
Wewe mke au mume ,wewe ndio mchawi wa ndoa yako Fanya haya ili
Uweze kuishi kwa furaha na Amani.1.Kuwa na mahusiano mazuri na Mungu
Tusisahau kumcha Mungu wewe mke au mume wengi huwa tunajisahau .Pale mke au Mme anapokosea tumuombee kwa Mungu arudi katika mstari .Uwe muislam au Mkristo ibada inakuhusu.
2.Uhuru wa kiuchumi.
Jamani maisha yamebadilika hivo basi kwenye ndoa tunatakiwa tusaidiane tusiwe tegemezi unakuta mwanamke umejibweteka hata hawazi mbali kuna Leo na kesho kila kitu unamtegemea mumeo akiwa hana na wewe taabani.Fanya hata Biashara ndogondogo uweze kujikimu na kujinunulia mavazi nasaa nyingine kuchangia katika chakula.Ukiwa tegemezi wanaume wa sasa wanakuchoka.Unakuta mwanamke kachoka hata chupi hana yani mavazi ya ndani na nje ni changamoto .Jamani tubadilike masuala mengine ni jukumu letu unakuta unategemea mume alipe kodi ya nyumba ,asomeshe watoto,avalishe,wakiumwa jamani sio kwa maisha haya maisha ni magumu.Ukiwa na shughuli/kazi mtasaidiana chumvi,sukari,unga etc vikiisha utanunua sio mpaka baba naniliu arudi.Vilevile hata kama mumeo akifa utakuwa unauwezo wakuihudumia familia.Jamani wababa wapendeni wake zenu mnawanyima matumizi mwisho wa siku anachoka na kutafuta danga la kumuwezesha kiuchumi.
3.Jipende katika maisha yako yote.
Unakuta mke baada ya kuolewa au mume baada ya kuoa anapoteza nuru hajipendi tena lakini enzi za mahusiano unakuta mwanamke msafi/mwanaume msafi.Jamani wanandoa tusipendeze wakati wa matukio mfano wa sherehe mbalimbali baada ya hapo unakua mchafu.Mke/Mme hukimbiana kutokana na tatizo la kutojipenda ndio mana mume anatafuta mchepuko na mke vivo hivo aliye smart.
4.Tujitahidi kukabiliana na mihemko.
Tusifanye maamuzi tukiwa na hasira sana au furaha sana.Ukikwazwa/kukasirika vumilia usionyeshe mpaka ukaanza kuongea maneno mabaya yakapelekea kuachana kabisa.Ukiwa na furaha jicontrol usije jikuta ukaanza kuropoka yasiyohusu kwa kifupi furahia ndani kwa ndani.
5.Tusipende kurudia makosa hasa pale tunapokanywa na wenza wetu.Vilevile tusipende kukumbushia makosa kwasababu hilo ni gubu.
6.Lugha nzuri kwa wenza.
Tuwe na lugha nzuri yenye mashiko siyo kazi kupayuka tu kama upo kijiweni na rafiki zako.
7.Tuache kuingia kwenye ndoa kwa shinikizo.
Utakuta watu wanaoana kisa umri unawatupa mkono,kwa vile fulani kaoa au kuolewa ,Kwa vile hali ngumu ya kiuchumi kwenu ndio waolewa baada ya miaka kadhaa mume akifirisika humpendi tena.
Follow me instragram @effypolly
tangazo hapa