tangazo hapa
24/08/2017Zijue faida na hasara za Mfumo wa kuchangiana kwa njia ya mtandao.
Mfumo wa kuchangiana kwa njia ya mtandao. Ni Mfumo ulioanzishwa katika nchi zilizoendelea na kusambaa katika nchi zinazoendelea.Mfumo huu umeanzishwa kwa ajili ya kutatua matatizo mbalimbali kama ya ugonjwa ,ada,mtaji au kusaidia maskini unatoa kama msaada mwenzio afanikiwe sio kwa ajiri ya kupata rejesho lakini mambo yamekua ndivyo sivyo kwa vijana wengi kuchukulia kama ajira na mtu hafanyi kazi anasubiri achangiwe.
Jinsi unavyofanya kazi
Mfumo unafanya kazi kwa matrix mbalimbali eg 2*2 matrix ,inamaanisha ukitoa mchango wako ni lazima utafute au utafutiwe watu wawili na wao wakuchangie na hao wawili ili wapande daraja lazima watafute wawili kwa hiyo Mfumo unatanuka unakua katika umbo la pembe Tatu huku wa juu akinufaika kwasababu huwezi panda daraja bila kumchangia wa juu mwishowe wa chini ndio anaeonyonywa akikosa wa kumchangia .Watu wengi wa juu wakipata hukimbia kuchangia tena ili Mfumo ufanye kazi vizuri ukichangiwa ni lazima uchangie.
Faida;
Husaidia watu kupata mtaji
Kukua kiuchumi
Kujuana na watu mbali mbali
Mfumo endelevu kwa waaminifu
Wa kwanza kuchangia ndio wa kwanza kunufaika
Hasara;
Watu wachache ufaidika
Mtu lazima awe na kipaji cha kushawishi
Kila mtu kwa sasa anajianzishia group la whatapps na kuchangisha bila kusajili serikalini
Maadmini wengi waanzilishi wa huu Mfumo siyo waaminifu
Wachangiaji siyo waaminifu wakipata michango hukimbia na Pesa za watu
Wajuu ndio unufaika zaidi ya wachini kwasababu wachini wapo katika changamoto ya kutopata michango.
Hakuna uwekezaji hivyo Pesa ya mtu Fulani anapewa mtu Fulani
Baadhi ya wanachama hurudisha Muamala pale wanapolipa kupitia mitandao ya simu kama Vodacom,Tigo etc wakidanganya wamekosea kutuma.
Kwanini Mfumo umekisiri kwa sasa licha ya serikali kupiga marufuku;
Hakuna ajira
Watu hawana mtaji
Watu kupenda njia za mkato ili watoke kimaisha
Watu wengi hawana uelewa jinsi Mfumo unavyofanya kazi
Toa maoni yako
tangazo hapa