Je umekata tamaa ya maisha? hili ndilo suluhisho.

Monday, 28 August 2017

Je umekata tamaa ya maisha? hili ndilo suluhisho.

tangazo hapa
Jinsi ya kukabili hali ya kukata tamaa.
Jinsi ya kukabiliana na hali ya kukata tamaa maishani.
Kukata tamaa ni hali ya kusitisha kufanya kitu kilichokua ndoto yako au malengo yako.Vijana,wazee,wanawake na wanaume wote hufikia hatua hii ya kukata tamaa katika masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii mfano kijana anapoamua kutojishughulisha  na chochote baada ya kukosa ajira aliyoitaka na kubakia kuwa mzigo katika jamii.
Kwanini watu hukata tamaa.
1.Kukatishwa tamaa na ndugu jamaa na marafiki.
2.Kufeli masomo
3.Kuachishwa kazi
4.kuwa maskini wa kipato na kifikra
Jinsi ya kuepuka hali ya kukata tamaa.
1.Kufanya sana ibada/Kuwa karibu na Mungu
2.Kujijua wewe ni nani,unahitaji nini katika maisha,njia gani ufanye ili ufanikiwe katika masuala yako mbalimbali. Kila mtu anajijua uwezo wake ,anachopendelea kufanya,udhaifu na nguvu yake.Endelea kuandika madhaifu na nguvu yako alafu baada ya wiki madhaifu futa ubakie na nguvu/uwezo wako  Endelea kupitia Mara kwa Mara mpaka yatakapokaa kichwani .Naimani utabadilika utatumikia ndoto zako.
3.Tafuta mda/sehemu tulivu ukae peke yako ujidiscuss masuala yanayokusibu alafu tafutia suluhisho mfano 1.nimekata tamaa sina ajira .Je vijana wote wameajiriwa? Kwani siwezi tumia elimu yangu au kipaji changu kujiingizia kipato?baada ya hapo utapata suluhu.mfano 2.Umeachwa na mke au mume je wewe ni wakwanza kuachwa? Kwani ukiwa umeachwa ndio utakua huishi?He wenzako waliochwa wamekufa? basi badilika.
4.Usikae peke yako .Mara nyingi ukikaa peke yako utadhidisha msongo wa mawazo tafuta ndugu ,jamaa au rafiki anaejielewa ukaenda kubadilishana mawazo inaweza ikawa tiba.
5.Kutafuta mtu aliyefanikiwa Mwenye ndoto kama zako ukaenda jifunza kwake atakuelekeza amepitia mangapi mpaka amefanikiwa kwahiyo utakua umejijenga vizuri kisaikolojia.
Hitimisho.
Watu wengi hukata tamaa za maisha hili ni gonjwa sugu.Ili tushinde hali hii ni lazima tufatane na walioshinda au waliothubutu.


tangazo hapa
Share :
Facebook Twitter Google+

 
Back To Top